al azhar

IQNA

IQNA – Wizara ya Awqaf ya Misri imetangaza tarehe rasmi za mitihani ya maandishi kwa washiriki wanaotaka kuiwakilisha Misri katika Mashindano ya 33 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu yatakayofanyika nchini humo.
Habari ID: 3482242    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/15

IQNA – Kituo cha Kiislamu cha Al‑Azhar nchini Misri kimeatangaza kuanza kwa msimu wa nne wa mradi wa majira ya joto wa Qur’ani unaolenga kuhudumia Kitabu Kitukufu na kufundisha Neno la Wahyi kwa njia ya malezi ya kiroho.
Habari ID: 3482240    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/15

IQNA – Kituo kipya cha Al‑Azhar cha kusomwa Qur’ani kwa njia ya mtandaoni, ambacho bado kiko katika siku zake za mwanzo za utendaji, kimepokelewa kwa mwitikio mpana na ushiriki mkubwa kutoka kwa maqari mashuhuri wa Qur’ani nchini Misri.
Habari ID: 3482194    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/03

IQNA – Taasisi ya Qur’ani ya Yemen iitwayo “Noon” imeukosoa msimamo wa hivi karibuni wa Kituo cha Kiislamu cha Al‑Azhar cha Misri dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ikisema kuwa unakinzana na wito wa Qur’ani Tukufu wa kusimama upande was haki na uadilifu.
Habari ID: 3482100    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/28

IQNA – Kituo cha Kiislamu cha AlAzhar nchini Misri kimehimizwa kufikiria upya msimamo wake kuhusu mashambulizi yanayoendelea ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, na pia kutafakari kwa makini kuhusu mustakabali wa ulimwengu wa Kiislamu na Umma wa Waislamu.
Habari ID: 3482090    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/03/26

IQNA – Chakula cha futari kimeandaliwa katika Msikiti Mkuu wa Al‑Azhar mjini Cairo kwa ajili ya wanafunzi wa kimataifa wa Chuo Kikuu cha Al‑Azhar.
Habari ID: 3481990    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/25

IQNA – Hafla maalumu imefanyika mjini Tehran siku ya Jumapili kutoa heshima kwa marehemu mwanazuoni mashuhuri Sheikh Ahmed Omar Hashem, aliyewahi kuwa Rais wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar cha Misri.
Habari ID: 3481907    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/09

IQNA – Kitivo cha Lugha cha Chuo Kikuu cha Al-Azhar nchini Misri kinaendeleza mradi mahsusi wa tafsiri na tarjuma unaolenga kuufikisha ujumbe wa Qur’ani Tukufu kwa mataifa mbalimbali duniani.
Habari ID: 3481798    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/13

IQNA – Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri pamoja na Radio ya Qur’ani ya taifa hilo, hivi karibuni wataanza mradi wa kurekodi qiraa mpya za Qur’an Tukufu.
Habari ID: 3481745    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/31

IQNA-Wakipita njia zilizozungukwa na majengo yaliyoharibiwa na vifusi, wanafunzi Wapalestina wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Gaza wiki hii wamerudi darasani kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili.
Habari ID: 3481692    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/21

IQNA-Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar katika mkoa wa Aswan, Misri, kimewatunuku zawadi na heshima maalumu dada watatu Wamisri waliokamilisha kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.
Habari ID: 3481651    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/12

IQNA – Sheikh Ahmed Al-Tayeb, Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri, amesisitiza kuwa kuzingatia kuhifadhi Qur'ani Tukufu ni msingi wa kujenga kizazi kipya cha vijana wenye uwezo wa kubeba ujumbe wa wema, rehema na amani – kiini cha risala ya Uislamu kwa ulimwengu.
Habari ID: 3481620    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/06

IQNA – Usajili wa wanafunzi wa kigeni wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar kwa mashindano ya 9 ya Kimataifa ya Qur’ani mjini Port Said umeanza rasmi.
Habari ID: 3481614    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/05

IQNA – Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Mielekeo ya Ugaidi kimeeleza wasiwasi wake kuhusu matumizi ya teknolojia ya Akili Mnemba (AI) na kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) kwa madhumuni ya kuajiri wafuasi wapya.
Habari ID: 3481599    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/01

IQNA – Jumuiya ya Kimataifa ya Wahitimu wa Al-Azhar imeandaa mashindano ya usomaji wa Qur’an ya “Sauti Njema” nchini Misri, tukio lililopokelewa kwa furaha na wanafunzi wa Al-Azhar kutoka mataifa mbalimbali.
Habari ID: 3481544    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/20

IQNA – Msikiti Mkuu wa Al-Azhar umetangaza uzinduzi wa matawi mapya 70 ya Taasisi ya Kuhifadhi Qur’ani ya Al-Azhar katika miji mbalimbali ya Misri.
Habari ID: 3481499    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/11

IQNA – Kisomo cha Qur’ani Tukufu kwa tarteel kilichorekodiwa na wanafunzi wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri kitaanza kurushwa hewani kupitia Idhaa ya Qur’ani ya Cairo kuanzia leo.
Habari ID: 3481496    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/10

IQNA-Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri kimezindua awamu ya kwanza ya mashindano ya kila mwaka ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu, maarufu kama Mashindano ya Sheikh Al-Azhar. Zaidi ya washiriki 150,000 wa kiume na wa kike kutoka mikoa mbalimbali ya Misri wanashiriki katika awamu hii ya mwanzo.
Habari ID: 3481476    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/06

IQNA – Sherehe maalum ya kuwatunuku wahifadhi wa Qur’ani Tukufu kutoka Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar imefanyika katika mkoa wa Giza nchini Misri.
Habari ID: 3481464    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/04

IQNA – Imamu Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri, Sheikh Ahmad al-Tayyib, amesema kuwa dunia inakumbwa na machafuko na ukosefu wa mantiki, hali ambayo chanzo chake ni kupuuzwa kwa maadili ya kidini na kiutu.
Habari ID: 3481456    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/03